Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM waitaka Iraq kuharakisha uchunguzi shambulio la kambi ya Ashraf

Wataalamu wa UM waitaka Iraq kuharakisha uchunguzi shambulio la kambi ya Ashraf

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa leo limeitaka serikali ya Iraq kubainisha hatma na majaliwa ya watu waliokuwa kwenye kambi yav Ashraf ambao ripoti zilisema kuwa walikuwa wametekwa.

Watu hao saba ambao walikuwa wakiishi kwenye kambi hiyo inaarifiwa kwamba walitekwa mwezi Septemba baada ya uvamizi uliofanywa ambao ulisababisha pia watu 52 kupoteza maisha.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakilaani na kuitaka serikali ya Iraq kuwajibika kutokana na kukosekana kwa taarifa kuhusiana na uchunguzi unaoendelea juu ya shambulio hilo.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali yaIraqkuharakisha uchunguziwa tukio hilo ili hatimaye iweze kujulikana hatma ya watekwa nyara hao na sababu zilizofanya kufanyika kwa shambulizi hilo.

Mmoja wa wataalamu hao Christof Heyns,amesema kuwa serikali ya Iraq inapaswa kuhakikisha kwamba uchunguzi huo unafanyika kwa haraka na kushindwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume mkataba wa kimataifa unaozingatia haki za kiraia na kisiasa.

Kambi hiyo iliyoko karibu na mji mkuu wa Baghad imekuwa ikihifadhi raia waIranwaliokimbia uhamishoni. Hadi sasa kambi hiyo ambayo ilianzishwa katika miaka 1980 imesaliwa na Wairan 3,000