Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yatoa msaada wa magari kwa tume ya uchaguzi ya Afghanistan:

UNAMA yatoa msaada wa magari kwa tume ya uchaguzi ya Afghanistan:

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Afghanistan UNAMA leo umetoa msaada wa magari 12 kwa tume huru ya uchaguzi nchini Afghanistan IECC na tume huru ya malalamiko ya uchaguzi IECC.

Kwa mujibu wa naibu mwakilishi na kaimu mkuu wa UNAMA Nicholas Haysom magari hayo yametolewa kwa ombi maalumu hata hivyo inataraji mwenendo mzuri wa tume hiyo wakati wa uchaguzi. Hayson ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi magari hayo iliyofanyika mjini Kabul.

Ameongeza kuwa UNAMA imeombwa kusaidia kukidhi mahitaji ya usafiri ma imefurahi kuwa na fursa ya kufanya hivyo kuisaidia tume ambayo ina jukumu muhimu la kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa wakati na kwa hadhi inayostahili.