Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha tamko la baraza la usalama kuhusu Yemen

Ban akaribisha tamko la baraza la usalama kuhusu Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tamko la baraza la usalama la tarehe 27 November ambalo limeahidi kusaidia katika mchakato wa amani wa mpito nchiniYemen ikiwamo kongamano la mjadala wa kitaifa.

Katibu Mkuu amesema baraza hilo linaendelea kusikitishwa na kuingiliwa au kucheleweshwa machakato wa mpito na kwamba baraza hilo liko tayari kuzingatia hatua za ziada ikiwa ni kuitikia matendo toka kwa mtu au vyama ambavyo vinakususdia kuingilia mchakato huo.

Bwana Ban amezitaka pande zote kushiriki katika mjadala wa kitaifa kwa imani na kuepuka vizuizi vya mchakato wa kipindi cha mpito. Ban pia amezihimiza pande zote husika kusuluhisha tofauti zao kwa njia ya majadiliano maridhawa ili kuwezesha watu waYemen kuendeleza mchakato.