Mashirika ya UM yaendelea kupeleka misaada kwa waathirika wa kimbunga Ufilipino:

11 Novemba 2013

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Kwa mujibu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP watu milioni 9.5 wameathirika na kimbunga hicho huku 400,000 wakitawanywa na kimbunga hicho na kulazimika kuishi katika makazi ya muda. WFP inasema kipaumbele chake kwa sasa ni kutoa msaada wa chakula na kiufundi ingawa operesheni za misaada ya kibinadamu inakabiliwa na changamoto kubwa kwani barabara nyingi hazipitiki kutokana na kuzibwa na kifusi

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

Kwa upande wake shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA kwa ushirikiano na serikali ya Ufilipino na wadau wengine wanaendelea kuwasaka manusura wa kimbunga hicho huku wakisafisha barabara kurahisisha uingizaji wa misaada. Kama anavyofafanua msemaji wa OCHA Jens Laerke

(CLIP YA JENS LAERKE)