Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya CEDAW yaimarisha nafasi ya wanawake katika utatuzi wa migogoro

Kamati ya CEDAW yaimarisha nafasi ya wanawake katika utatuzi wa migogoro

Nchi ambazo zimesaini mkataba wa kimataifa wa kupinga aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake, CEDAW zimehimizwa kuhakikisha zinazingatia haki za wanawake wakati na hata baada ya mizozo na pia zinapochangia katika ulinzi wa amani. Alice Kariuki na ripoti kamili.

(Ripoti ya Alice)

Maelekezo hayo yamo kwenye nyaraka ya aina yake iliyopitishwa na Kamati inayosimamia CEDAW huko Geneva ambamo pia imetaka vikundi vya kiraia vyenye silaha ikiwemo kandarasi za ulinzi wanawajibishwa kwa uhalifu dhidi ya wanawake. Nicole Amelia ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema nyaraka hiyo inatambua dhima ya wanawake katika kuzuia mizozo na hata ujenzi wa nchi baada ya vita. Amesema uzoefu wa wanawake mara nyingi hutupiliwa mbali na hata ushiriki wa wanawake kihistoria kwenye utatuzi wa migogoro umekuwa ni wa chini sana.

(Sauti ya Nicole)

Nyaraka hiyo ilipitishwa na kamati hiyo tarehe 18 mwezi huu siku ambayo pia baraza la usalama lilipitisha azimio la kutambua umuhimu wa wanawake katika utatuzi wa migogoro.