Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi nyingi zasaini mikataba ya UM

Nchi nyingi zasaini mikataba ya UM

Zaidi ya mataifa 40 yanaripotiwa kupiga hatua kwa kuidhinisha ama kusaini mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo ukiwemo ule unaohusu ulinzi kwa watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji na mateso mengine.

Hayo yameelezwa kufikiwa wakati wa kikao cha baraza la Umoja wa Mataifa kilichofanyika New York na kuhudhuria na viongozi wa mataifa mbalimbali wanachama.

Akijadilia kwa kina msaidizi wa Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya sheria , Patricia O’Brien amesema kuwa hatua hiyo inatoa nukta mpya katika historia ya Umoja wa Mataifa.

Mwanadiplomasia huyo ambaye alikuwa akizungumza wakati wa kufungwa kwa kikao hicho amesifu mafanikio hayo ambayo ameyaelezea kama ni ishara ya kutia matumaini ambayo inabainisha namna nchi wanachama zilivyokuwa tayari kufanya kazi kwa umoja.