WFP yaweza kupunguza usaidizi wa chakula huko DR CONGO

22 Oktoba 2013

Kutokana na uhaba wa fedha Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limelazimika kupunguza huduma zake maeneo kadha nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC hata baada ya kuwasaidia watu milioni 3.6 kati ya mwezi Septemba mwaka 2012 na Juni mwaka huu. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(Ripoti ya Assumpta)

 WFP inasema kuwa hali hiyo huenda ikawaathiri watoto wa shule, wakimbizi , wanaorejea makwao na wale waliokuwa wamepiga hatua, na ni pigo kwa hatua  zilizofikiwa hasa za kujitegemea. WFP inasema kuwa ikiwa fedha hazitapatikana kwa haraka haitaendela kuwahudumia watu 300,000 ambao ni wakimbizi wa ndani mkoani Kivu Kaskazini na ambao wamekuwa wakipokea msaada nusu kwa muda wa miezi sita iliyopita. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(Sauti ya Byrs)

Kutokana na kuchacha mwa mzozo eneo la Irumu Kusini, watu 80,000 wana mahitaji ya chakula. Hata hivyo idadi hii huenda ikaongezeka hadi watu 120,000 na hadi watu 150,000. WFP haina njia za kukabilina na hali hii na kwa sasa inatumia chakula kutoka kwa huduma  zingine.

 Matokeo ya utafiti kuhusu usalama wa chakula uliofanywa kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini mwezi Juni mwaka 2012 yanaonyesha kuwa asilimia 61 ya familia mkoani humo hawana uhakika wa chakula.