Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Aliyoyatetea Mwalimu Nyerere yako dhahiri hadi sasa: Jamaica

Aliyoyatetea Mwalimu Nyerere yako dhahiri hadi sasa: Jamaica

Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi mwenye dira na yale aliyoyatetea tunayashuhudia sasa na tunayapigia chepuo katika ajenda ya baada ya mwaka 2015, ni kauli ya mwakilishi wa kudumu kwenye Umoja wa Mataifa wa Jamaica Courtenay Rattray aliyotoa wakati akihutubia kwenye tukio maalum la Kumuenzi Baba wa Taifa la Tanzania kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, siku ya Jumatatu.

Balozi Rattray ametolea mfano wa falsafa ya Ujamaa ambayo amesema Mwalimu Nyerere aliianzisha kwa ajili ya Taifa lake ili kuweka usawa wa kiuchumi na kijamii ambayo pia inajenga maendeleo na jamii shirikishi.

(Sauti ya Balozi Rattray)

Mwakilishi huyo wa kudumu wa Jamaica akazungumzia pia hatua ya Mwalimu Nyerere ya kuendeleza lugha ya Kiswahili..

(Sauti ya Balozi Rattray)

Amegusia pia uhusiano kati ya Waziri Mkuu wa zamani wa Jamaica Michael Manley na Mwalimu Nyerere, ambao amesema uliimarisha uhusiano kati ya nchi zao na hata katika kuimarisha ushirikiano wa nchi za Kusini.