Bi. Robinson alaani shambulio dhidi ya helikopta ya MONUSCO huko Rumangabo

12 Oktoba 2013

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa eneo la Maziwa Makuu barani Afrika, Mary Robinson ameshutumu shambulio dhidi ya helikopta ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo, MONUSCO kwenye eneo la Rumangabo, Kivu Kaskazini,  linaloshikiliwa na waasi wa kikundi cha M23. Taarifa mjumbe huyo kwa waandishi wa habari imesema imemkariri Bi. Robinson akishutumu vikali kitendo hicho ambacho amesema kinatishia usalama wa watendaji wa MONUSCO. Amekumekumbusha viongozi wa M23 kuwa kitendo chochote kitakachokwamisha majukumu ya MONUSCO kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama namba 2098  hakikubaliki.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud