Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wengi wanamatatizo ya kuona-WHO

Watu wengi wanamatatizo ya kuona-WHO

Takwimu zilizotolewa na shirika la afya ulimwenguni WHO zinaonyesha kuwa karibu watu milioni 39 dunia ni walemavu wa kuona.

Kadhalika watu wengine milioni 246 wanakabiliwa na matatizo ya kuona kiasi ama wanamatatizo makubwa ya kuonaWHO imesema kuwa bado haijajulikana hadi sasa ni chanzo cha matatizo ya watu kutokuona.Lakini kwa upande mwingine WHO imesema kuwa zaidi ya asilimia 10 ya watoto wanapoteza kuona kutokana na matatizo ya utapiamlo.

Taarifa hizo zimetolewa katika wakati ambapo dunia inaathimisha siku ya kuona duniani.