Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Cameroon yafanya kampeni ya chanjo kufuatia kuzuka homa ya manjano

Cameroon yafanya kampeni ya chanjo kufuatia kuzuka homa ya manjano

Serikali ya Cameroon imefanya kampeni ya chanjo ya halaiki na kuwafikia asilimia 94 ya watu wapatao laki sita na elfu sitini na tatu katika wilaya zilizopo kwenye hatari ya maambukizi ya homa ya manjano.

Kampeni hiyo ilifanyika kati ya Agosti 27 na Septemba 1 katika eneo la Littoral, kufuatia visa viwili vya homa ya manjano kutoka eneo hilo kuthibitishwa katika maabara ya Shirika la Afya Duniani, WHO mjini Dakar, Senegal, mnamo mwezi Aprili 2013.

WHO imekuwa ikishirikiana na mamlaka za afya kuchunguza na kuitikia mkurupuko huo wa homa ya manjano, ambao ulidhaniwa kuanza mnamo mwaka 2012 katika maeneo ya Kaskazini Magharibi, Magharibi na Kusini Magharibi.