Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na ghasia zilizojiri Misri Jumapili

Ban asikitishwa na ghasia zilizojiri Misri Jumapili

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameshutumu vikali ghasia zilizoibuka Jumapili nchini Misri wakati wa maandamano na kusabaisha vifo vya watu zaidi ya 50 huku akituma rambirambi kwa wafiwa na kutakia ahueni ya mapema waliojeruhiwa kwenye zahma hiyo.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Bwana Ban amerejelea wito wa kutaka maandamano yawe yanafanyika kwa amani kama alivyosisitiza Ijumaa kabla ya maandamano hayo bila kusahau kuheshimu uhuru wa kukusanyika na siasa jumuishi. Ameendelea kusisitiza pia umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu ikiwemo za wale waliomo gerezani pamoja na utawala wa kisheria, mambo ambayo amesema ni msingi wa kipindi cha mpito chenye demokrasia nchini Misri. Wakati huo huo Katibu Mkuu ameshutumu mashambulio ya leo huko Misri dhidi ya maeneo ya kijeshi na askari, ambayo yameripotiwa kusababisha vifo vya watu wanane na wengine kadhaa kujeruhiwa.