Tanzania iwe makini na uchimbaji wa madini ya Urani: Wataalamu

4 Oktoba 2013

Jopo la wataalamu wa masuala ya nuklia na wale kutoka mtandao wa madini ya Urani, wamesema Tanzania iwe makini katika uchimbaji wa Urani yaliyogunduliwa huko Dodoma na Ruvuma ili kuepuka matatizo yanayoweza kuibuka iwapo hatua stahili hazitachukuliwa. Kutoka dsm, George Njogopa na taarifa zaidi

(Taarifa ya George)

Wito huu umekuja katika wakati ambapo serikali yaTanzaniainaanzisha juhudi za kuchumba madini hayo yalyoko Wilayani Namtumbo, Mkoani Ruvuma Kusin mwaTanzaniana Wilayani Bahi MkoaniDodoma. Wataalamu hao ambao wamekutana nchini kwa kongamano la wiki moja, lililoanzia huko Wilayani Bahi na kisha jijiniDar es salaam, wametahadharisha madhara ya kiafya yanayoza kuwakumba wananchi iwapo zoezihilolitaendeshwa kwa pupa. Akiweka mkazo zaidi katikahilo,Profesa Andreas Nidecker, kutoka Mtandao wa Kimataifa wa Wanafizikia wa Kuzuia vita vya Kinyuklia, aliitakaTanzaniakujifunza kutoka mataifa mengine ambayo yamekumbana na madhara yatokanayo na madini ya Urani.

 “Watu katika mataifa ambayo huzalisha kwa wingi Urani wamekumbana na matatizo zaidi kuliko faida za kiuchumi. Tatizo la hivi karibuni la Yokoshima limedhibitisha kitisho kilichoko kwenye matumizi ya nyuklia”.

Bwana Antony Yamunda ambaye ni miongoni mwa wale waliomstari wa mbele kupingana na uchimbaji huo anasema kuwa.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kongamano hilo la kimataifa, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Hussein Mwinyi pamoja na kukiri athari zitokanazo na uchimbaji wa madini hayo, lakini aliongeza kuwa…