Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tujitahidi kulinda haki za wahamiaji wote: Ban

Lazima tujitahidi kulinda haki za wahamiaji wote: Ban

Mara nyingi wahamiaji huishi maisha ya hofu ya kunyanyswa kwa kile wanachoitwa “wengine”, kwa kutopata haki za kisheria na pasi zao za kusafiria kushikiliwa au kutopewa mishahara na waajiri wao.

Hayo yamesema Alhamisi na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon kwenye mjadala wa ngazi ya juu kuhusu uhamiaji wa kimataifa na maendeleo.Ban ameongeza kuwa dunia haiwezi kunyamza kimya.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

“ hatuwezi kukaa kimya , tunahitaji kutokomeza mifumo yote ya ubaguzi dhidi ya wahamiaji, ikiwemo inayohusiana na mazingira ya kazi na mishahara. Tunahitaji kuanzisha mifumo zaidi ya usalama kwa wahamiaji na kupata mbadala wa kuwaweka mahabusu wahamiaji”.

Ban ameongeza kuwa taswira ya uhamiaji inabadilika, na leo hii wahamiaji wanaingia na kutoka sehemu mbalimbali kuliko siku za nyuma. Karibu nusu ya wahamiaji wote ni wanawake na kila mmoja kati ya 10 ni muhamiaji wa chini ya umri wa miaka 15.