Uzalishaji wa mazao ya nafaka ni wa kuridhisha kwa kipindi cha 2013-2014: FAO

3 Oktoba 2013

Hali ya usambazaji wa mazao ya nafaka katika kipindi cha mwaka 2013-2014 kinaelezwa kuwa ni cha kuridhisha pamoja na kuwepo viashiria vinavyoeleza kuwepo uwezekano wa kuanguka kwa  uzalishaji wake katika soko la dunia.

Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika la chakula duniani FAO, pamoja na kutegemea kujitokeza mabadiliko kiasi juu ya mazao ya nafaka ,lakini uzalishaji wa mazao hayo katika msimu unaokuja utakuwa mkubwa kushinda kiwango kilichorekodiwa mwaka uliopita 2012.

.Alice Kariuki na taarifa kamili

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Wakati takwimu za FAO zikieleza kupanda kwa uzalishaji huo wa mazao ya nafaka, kwa upande mwingine, FAO imeonyesha kuwa, kiwango cha bei ya chakula kilishuka katika kipindi cha mwezi Septemba kutokana na kile ilichoeleza kuwa ni kuanguka kwa haraka kwa bei mazao ya nafaka katika soko la kimataifa.

Lakini bei ya vitu kama nyama, mafuta, maziwa na sukari ilipanda kwa kiasi.

Ripoti hiyo inayonyesha mwelekeo wa mambo ambayo pia inapima mabadiliko ya kila mwezi ya bei ya bidhaa katika soko la kimataifa,imesema kwa sehemu nyingine kumejitokeza mabadiliko makubwa ikilinganishwa na rekodi iliyochukuliwa kipindi cha mwaka 2009 au 2010.

FAO inatazamiwa kuwa na mkutano wa ngazi za mawaziri jumatatu ijayo Mjini Roma, Italia kwa ajili ya kujadilia bei ya chakula katika soko la kimataifa.