Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtindio wa ubongo si kigezo cha kunyimwa haki ya kupiga kura: Wataalam

Mtindio wa ubongo si kigezo cha kunyimwa haki ya kupiga kura: Wataalam

Watu wenye mtindio wa ubongo hawapaswi kunyimwa hakiyaoya kupiga kura. Ni maoni ya Kamati ya wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa baada ya kuchunguza kesi ya raia sita waHungaryambao wamepokonywa hakiyaoya kupiga kura baada ya kuwekwa chini ya uangalizi wa kisheria. Watu hao waliwasilisha malalamikoyaombele ya kamati ya haki za watu wenye ulemavu mjiniGeneva, baada ya kushindwa kupiga kura kwenye uchaguzi wa bunge na manispaa nchini mwao mwaka 2010. Walisema kuwa walikuwa na uwezo wa kuelewa siasa na kushiriki kwenye uchaguzi na kwamba kuzuiwa kwao ambako hakukuzingatia msingi wa ulemavu wao na uwezo wao binafsi hakukuwa  halali. Hata hivyo serikali yaHungaryimesema kuzuiwa kwao kulitokana na kifungu katika katiba na kwamba hivi sasa kwa mujibu wa katiba mpya ni Jaji peke ndiye anayeweza kuamua mtu apige kura au la. Kamati hiyo ikiwa na wataalamu huru 18 imesemaHungaryhaikupaswa kufanya hivyo na kwa mantiki hiyo ipitishe sheria inayowapa haki wenye mtindio wa ubongo haki ya kupiga kura na iweke mazingira rafiki kufanikisha hatua hiyo.