Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa nafaka Afrika wakutana Mombasa

Wataalamu wa nafaka Afrika wakutana Mombasa

Zaidi ya viongozi 250 kutoka bara la Afrika wakiwemo wakurugenzi kutoka sekta za kibinafsi, wakulima , wafanyibiashara , mashirika yasiyokuwa ya serikali , taasisi za kifedha, waakilishi wa serikali na watunza sera watakusanyika mjini Mombasa nchini Kenya kati ya Oktoba mosi na Oktoba tatu kujadili masusla yayoathiri sekta ya nafaka barani Afrika. Jason Nyakundi na taarifa kamili:

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mkutano huu unajiri wakati kila jitihada zinaelekezwa kuhakikisha kuwa bara la Afrika limejilisha na hata ulimwengu wote. Bara la Afrika lina takriban watu bilioni moja likiwa na ukubwa wa kilomita milioni 30.2 mraba ambapo ndipo yaliyo mataifa 10 yanayokuwa kwa kasi zaidi duniani kwa hadi asilimia sita. Kando na hilo bara la Afrika lina vijana wengi, mapato yanayoongezeka pamoja na sekta za kibinafsi zinazozidi kukua hali ambayo inatoa fursa nzuri na mzingira bora kwa wawekezaji. Kwenye mkutano wa mwaka huu wajumbe wataangazia masuala ambayo yatachangia kuwepo ushirikiano kati ya sekta za umma na zile za kibinafsi na kuchangia kuwepo uwekezaji zaidi kwenye sekta ya nafaka. Masuala kuhusu uvumbuzi na matumizi ya teknolojia na jitihada za kuongeza uwekezaji kwenye kilimo barani Afrika yatajadiliwa.