Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua nzuri zimepigwa na FAO: Ripoti ya DFID:

Hatua nzuri zimepigwa na FAO: Ripoti ya DFID:

Shirika la chakula na kilimo FAO limepiga hatua katika miaka miwili iliyopita lakini bado kuna mengi ya kufanya, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na kuchapishwa na idara ya Uingereza ya maendeleo ya kimataifa DFID. Alice Kariuki na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Ripoti hiyo kuhusu FAO imekuja kukiwa kumepita miaka miwili tangu taaisi hiyo ya Uingereza kutoa ripoti yake ambayo ilipewa kichwa cha habari kuwa “ thamani ndogo ya fedha kwa walipa kodi wa Uingereza.

Ripoti hiyo imetambua kile ilichokiita changamoto ambazo FAO inakabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa mabadiliko ya kimifumo. Lakini kwa upande mwingine ripoti hiyo imetambua hatua kubwa zilizopigw a na FAO ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita.

Imesema  kuwa mabadiliko hayo yanakusudia kuonyesha mchango wa wafanyakazi wa FAO namna wanavyotoa kipaumbele kutekeleza miradi yenye shabaha ya kukabiliana na tatizo la njaa duniani.

Aidha ripoti hiyo imepongeza hatua mpya inayotekelezwa na FAO kupitia miradi yake ya kukabiliana na njaa na eneo moja wapo ililolitaja ni lile linalotambulika sasa kama “ miradi inayolingana na thamani ya hela”