Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahitaji msaada kuimarisha miundombinu: Sudani Kusini

Tunahitaji msaada kuimarisha miundombinu: Sudani Kusini

Makamu wa rais wa Sudan Kusini James Igga ni miongoni viongozi waliohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema nchi yake inahitaji msaada mkubwa jumuiya ya kimataifa hususani katika miundombinu baada ya mapigano kuathiri kwa asilimia kubwa njia za usafiri. Katika mahojiano maalum na idhaa hii kandoni mwa mkutano huo Bwana Igga amesema ni vigumu kuwafikia wanohitaji misaada isipokuwa kwa njia ya anga pekee

SAUTI

Nchini mwetu kwa kuwa ndio tumeondokana na vita ni muhimu watu wenye nia njema wasaidie watu wa Sudan Kusini katika muiundiomibinu kwa hata misaada ikiwepo namna ya kuifikisha kwa walengwa ni ngumu hakuna barabara,reli ni kikwazo kwahiyo jumuiya ya kimataifa ijihusishe kutusaidia kimiundombinu ,kifedha kiuchumi, nafikiri twaweza kupunguza mateso ya watu

Kuhusu utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia katika muktadha huu akasema.

Tunafanya kila tuwezalo kwa mfano katika usawa wa kijinsisa mwaka uliopita ushiriki wa wanawake katika siasa ulikuwa asilimia 25 sasa hivi imefika 35 na hii ni njia kuelekea kutekeleza malengo haya, tunanuia pia kupunguza vifo vya watoto, katika elimu ya msingi tunapamabana na ndoa za umri mdogona huu ni utashi wa kuboresha mambo