Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sikuagiza sanamu ya Waziri Mkuu ing’olewe” Pillay

Sikuagiza sanamu ya Waziri Mkuu ing’olewe” Pillay

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema Kamishna mkuu Navi Pillay kamwe hakutoa maoni yoyote kuhusu sanamu ya Waziri Mkuu DS Senanayake na kwamba hakuna mahali popote wakati wa ziara yake nchini humo ambapo aliagiza sanamu hiyo iondolewe. Kauli  ya ofisi hiyo imetolewa baada ya kusambaa kwa taarifa hizo potofu ambapo tayari Bi. Pillay ameiandikia serikali yaSri Lankaakiomba kufutwa kwa madai hayo huku akitaka kufanyiwa marekebisho haraka ya taarifa hizo ambazo amesema zimeleta tashwiswhi kubwa nchini humo. Wakati huo huo Bi. Pillay atawasilisha ripoti ya ziara yake nchini Sri Lanka mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa tarehe 25 mwezi huu.