Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mnahitajika kuandaa mustakhbali wa dunia hii, Ban awaeleza washiriki wa kikao cha viongozi

Mnahitajika kuandaa mustakhbali wa dunia hii, Ban awaeleza washiriki wa kikao cha viongozi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza kwenye kikao cha viongozi kijulikanacho kama Global Compact Leaders na kusema kuwa wao ndio wanaotegemewa katika kuandaa mustakhbali endelevu wa dunia. Ripoti ya Joseph Msami inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Joseph Msami)

Vitendo vyenu vinahesabika na tunawahitaji ninyi muwe waandaji wa mustakhbali endelevu, ni kauli ya Bwana Ban kwa washiriki wa kikao hicho akieleza kuwa amefarijika zaidi kwa kuona uwakishili mkubwa wa wanawake. Amesema uwezeshaji wanawake ni kitovu cha maendeleo endelevu, tulivu na siri ya mafanikio ya jamii zilizosonga mbele.

Ameongeza kuwa ni lazima kuvunja mipaka na kuhakikisha sasa ushiriki wa wanawake siyo tu kuongeza idadi yao darasani bali pia washike nyadhifa muhimu. Bwana Ban amesema makundi yote yanahitajika ili kuwa na njia endelevu ya kuunganisha ukuaji wa uchumi, usawa na haki ya kijamii na hata udhibiti bora wa mazingira.

(Sauti ya Ban)