Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCTAD yahimiza uanzishwaji wa kilimo mchanganyiko

UNCTAD yahimiza uanzishwaji wa kilimo mchanganyiko

Ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na biashara na maendeleo UNCATD, imesema nchi maskini pamoja na zile tajiri ambazo hujishughulisha na kilimo cha aina moja zinapaswa kubadilisha mkondo na kuhamia katika kilimo chenye mkusanyiko mwingi wa mazao.

UNACTD imesema kuwa, nchi hizo pia zinapaswa kuchukua jukumu la kupunguza matumizi ya pembeb jeo na kuanza kuwaunga mkono wakulima wadogo wadogo.

Ripoti hiyo ya mwaka 2013 iliyokuwa na kichwa cha habari, biashara na mazingira imeonya kuwa kuendelea kuziachia nchi maskini kukabiliana na matatizo ya kimazingira ni jambo la hatari.

Imesema mambo kama umaskini wa vijijini, kujitokeza kwa tatizo la njaa duniani, pamoja na tatizo la ongezeko la idadi ya watu, ni mambo ambayo yanapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano wa pamoja.