Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mizozo kugharimu masomo ya mamilioni ya watoto duniani kote: Zerougui

Mizozo kugharimu masomo ya mamilioni ya watoto duniani kote: Zerougui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya watoto na mizozo ya kivita, Leila Zerrougui amesema mizozo inayoendelea maeneo mbali mbali duniani inasababisha mamilioni ya watoto washindwe kwenda shule kuhudhuria masomo, jambo ambalo ni haki yao ya msingi. Ripoti ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.

(Ripoti ya Grace)

Mbele ya kikao cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa huko The Hague, Bi. Zerrougui ametaja mizozo na sintofahamu zinazoendelea duniani akigusia Somalia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Syria. Amesema shule zinafunguliwa lakini mamilioni ya watoto kwenye maeneo hayo watakosa fursa ya kushiriki masomo kutokana na hofu ya vita.

Amesema katika maeneo hayo yote ukiukwaji wa haki ni mkubwa akisema huko Somalia kuna idadi kubwa ya watoto wanaohusishwa kwenye vikundi vyenye silaha. Amesema matumaini yaliyojitokeza Jamhuri ya Afrika ya Kati na DRC yametumbukia na hata awtoto waliokuwa wameondolewa kwenye vikundi vya waasi wametumikishwa tena.