Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji unakwamishwa na uchumi na sera dhaifu- Mkuu UNCTAD

Uwekezaji unakwamishwa na uchumi na sera dhaifu- Mkuu UNCTAD

Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD, Mukhisa Kituyi ameonya kwamba mpango wa wa kufufua uwekezaji kimataifa unasuasua kufuatia wawekezaji kusita kupanua biashara katika wigo wa uchumi unaolegalega na kutokuwa na uhakik wa sera. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya baraza hilo kuhusu uwekezaji

Akizungumza katika kongamano la 17 la uwekezaji sawia na biashara (CIFIT) linaloendelea Xiamen China, Bwana Kituyi amesema licha ya kusuasua kwa mpango huo yako mafanikio makubwa akiangazia yale ya mwaka 2012 ambapo ameainisha kwamba nchi zinazoendelea kwa mara ya kwanza zimevutia uwekezaji wa nje kuliko zile zilizoendelea kwa kupokea asilimia 52 ya wawekezaji.

Akiwa nchini China ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuanza rasmi kwa kazi yake mwanzoni mwa mwezi huu, Katibu huyo Mkuu wa UNCTAD amekutana na viongozi kadhaa wa serikali ya nchi hiyo na wale waliowakilisha nchi zao katika kongamano hilo na kuzungumza nao kuhusu kuimarisha uhusiano wa kimaendeleo na kujadili kuhusu namna ya kusaidia nchi zinazoendela katika maeneo kadhaa ikiwamo misaada ya kiufundi.