Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka kuweko shabaha ya pamoja kukabili tatizo la ukosefu wa kazi duniani

UM wataka kuweko shabaha ya pamoja kukabili tatizo la ukosefu wa kazi duniani

 Jamii ya kimataifa imehimizwa kuweka zingatio la pamoja kwa kushagihisha mifumo yake ili hatimaye iweze kufaulu kukabili tatizo la ajira linaloiandama dunia kwa sasa.

 Kwa mujibu wa rais wa baraza la uchumi na la kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC Bwana Lazarous Kapambwe kuna haja kubwa kwa jamii ya kimataifa kufungamanisha mifumo yake ya ukuzaji uchumi na mikakati ya kukabili tatizo la ukosefu wa kazi.

Bwana Kapambwe, amesisitiza pia ni muhimu kuanisha njia mjarabu zitakazosaidia kutatua tatizo la ukosefu wa kazi kwa kuangalia malengo ya baadaye na siyo kuweka zingatia la wakati huu pekee.

Kwa maoni yake anasema kuwa tatizo la mkwamo wa kiuchumi iliyokumba dunia sasa limechukua sura nyingine na kuhamia kwenye mkwamo wa dunia wa ukosefu wa kazi.