Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama wa chakula ukanda wa Sahel bado mbaya:FAO

Hali ya usalama wa chakula ukanda wa Sahel bado mbaya:FAO

Takribani wakazi Milioni Kumi na Mmoja katika ukanda wa Sahel bado hawana uhakika wa chakula, hiyo ni taarifa ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO iliyotolewa leo ikiwa ni tahadhari wakati huu ambapo familia zimetumia akiba yote ya chakula huku zikikabiliwa na bei ya juu za vyakula wakati wakisubiria msimu ujao wa mavuno. Ripoti ya Flora Nducha inafafanua zaidi.

(TAARIFA YA Flora Nducha)

FAO imeitolea wito jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada ya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wadogo wadogo pamoja na wale walioko kwenye mazingira magumu ikiwemo wale wa eneo la Kusini mwa Sahara. Pamoja na ombi hilo FAO la kutaka msaada wa zaidi ya dola za Marekani Milioni 113 ili kuzisaidia watu Milioni Sita dani ya mwaka huu pekee, lakini hadi sasa imefaulu kukusanya kiasi cha dola 19 ikiwa ni asilimia 17 tu ya ombi lake jumla. Kumekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya kuendelea kuanguka ustawi wa kibinadamu kwenye eneo hilo huku watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ndiyo wanaotajwa kuwa katika wakati mgumu kabisa.FAO imeanzisha juhudi za kukusanya mafungu ya fedha kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kwa kuwapatia misaada ya pembejeo na mahitaji mengine ya muhimu.