UNAMID inasaidia kusafirisha kwa ndege raia wa Darfur Mashariki:

22 Agosti 2013

Kama sehemu ya juhudi zake za kusaidia raia walioathirika na machafuko ya jamii tofauti, mpango wa pamoja wa kulinda amani Darfur wa Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID umesaidia kusafirisha kwa ndege raia 300 mwezi huu kutoka El Daein Mashariki mwa Darfur hadi Abu Karinka karibu kilometa 50 Kaskazini Mashariki mwa El Daein. Zaidi ya hapo Jana tarehe 21 Agosti UNAMID imetoa msaada wa kiufundi kusaidia kuwasafirisha wawakilishi wa makabila ya Rezeigat na Ma’alia kwenda Al Tawisha Kaskazini mwa Darfur ili kushiriki kwenye utiaji saini makubaliano ya kusitisha mapigano Mashariki mwa Darfur.

Hali hivi sasa Mashariki mwa Darfur ilisababishwa na mgogoro wa ardhi ambao bado hauajapata suluhu na kukabiliana na hali hiyo UNAMID imeongeza uwepo wake na doria katika eneo hilo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter