Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto lazima walindwe nchini Syria:UNICEF

Watoto lazima walindwe nchini Syria:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto ni lazima walindwe , baada ya ripoti kwamba silaha za kemikali zimetumika kwenye machafuko yanayoendelea nchini Syria ambayo yameshasababisha vifo vingi vikiwemo vya watoto.

Kwa mujibu wa UNICEF mashambulizi dhidi ya raia wakiwemo watoto yaliyofanyika nje kidogo ya Damascus yanasikitisha na kitendo hicho cha kikatili ni lazima kiwe kumbusho kwa pande zote zenye ushawishi katika vita hivyo kwamba machafuko yamefurutu ada na watoto wameteseka vya kutosha.