Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yapongeza kuanza kwa mkataba mpya unaohusu usafiri wa majini

ILO yapongeza kuanza kwa mkataba mpya unaohusu usafiri wa majini

Shirika la kazi duniani ILO, limesema kuwa wakati mkataba wa wanamaji wa mwaka 2006, ukitarajia kuanza kufanya kazi August 20, nuru mpya wa matumaini inafunguka kwa watumishi wanaotumia muda wao mwingi wakiwa kwenye vyombo vya baharini.

ILO inasema kuwa kuanza kazi kwa mkataba huo kunamaanisha kuwa, sasa maelfu ya wafanyakazi watakuwa wakiendesha majukumu yao katika mazingira salama na uhakika zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Guy Ryder hata hivyo ameyatolea mwito baadhi ya mataifa kuidhinisha mkataba huo ambao umeuita kuwa ni wa kihistoria katika sekta ya usafiri wa kwenye maji.

Mkataba huo mpya unatazamiwa kuanza kazi rasmi August 20 lakini hata hivyo utalazimika kwanza kuidhinishwa na nchi wanachaa wa shirika hilo zipatazo 30.