Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awapa heko watu wa Mali kwa uchaguzi wa urais

Ban awapa heko watu wa Mali kwa uchaguzi wa urais

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ametoa heko kwa mamlaka na watu waMalikwa kuendesha uchaguzi wa urais kwa njia ya ufanisi mnamo Julai 11, 2013.

Wakati raia wa Mali wakisubiri kuthibitishwa kwa matokeo ya uchaguzi huo na Mahakama ya Kikatiba, Bwana Ban amempa hongera Bwana Ibrahim Boubacar Keїta kwa kuchaguliwa kuwa rais wa taifa la Mali, kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya awali.

Katibu Mkuu pia amemsifu Bwana Soumaïla Cissé, ambaye ameibuka wa pili katika uchaguzi huo kwa kukubali matokeo ya uchaguzi, na kusifu kujitoa kwake kuunga mkono kanuni za demokrasia.

Bwana Ban ameahidi uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa katika hatua itakayofuata katika harakati za kuweka utulivu na kuimarisha amani, zikiwemo kuunga mkono mazungumzo jumuishi na maridhiano, pamoja kuandaa uchaguzi wa kitaifa wa ubunge.