Kushamiri ghasia Sudan Kusini kwatia shaka UM

Kushamiri ghasia Sudan Kusini kwatia shaka UM

Serikali ya Kusini mwa Sudan imetakiwa kuweka mikakati ya kukabiliana na vitisho vinavyoharisha usalama wa eneo hilo, ambavyo vinaendeshwa na makundi ya askari waaasi.

Wito huo umetolewa na mratibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na eneo hilo David Greasly ambaye amesema Umoja wa Mataifa una mashaka makubwa na mwenendo wa mambo hasa kutokana na kuendelea kushamiri kwa matukio ya ghasia.

Amezitaka mamlaka za Sudan Kusini kukabiliana na hali hiyo kwa kuzingatia sheria za kimataifa. Kwa mujibu wa naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq kumekuwa na mapigano ya mara kwa mara katika maeneo kadhaa yanayohusisha vikosi kadhaa vya msituni.