Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawasiliano changamoto kubwa Tanzania ikielimisha uma kuhusu unyonyeshaji:Dk Rashid

Mawasiliano changamoto kubwa Tanzania ikielimisha uma kuhusu unyonyeshaji:Dk Rashid

Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kilele cha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha, nchi mbalimbali zimetumia wiki hii katika kuelimisha uma na kutathimini hali ya unyonyeshaji wa watoto wadogo ambao kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, wanapaswa kunyonyeshwa kwa miezi sita ya mwanzo bila kupewa lishe nyingine.

 NchiniTanzaniazoezi la kuelimisha uma limefanyika licha ya kukabiliwa na vikwazo kadhaa ikiwamo mawsiliano. Ungana na mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Matifa  Joseph Msami,  katika mahojiano maalum na naibu waziri wa afya wa nchi hiyo Dk Seif Rashid anayeanza kueleza kampeni ya uelimishaji inavyofanyika.