Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kuhusu jinsia na huduma za afya kujadiliwa na wataalamu Botswana

Elimu kuhusu jinsia na huduma za afya kujadiliwa na wataalamu Botswana

Wataalamu na watunga sera kutoka Mashariki na Kusini mwa Afrika watakutana mjini Gaborone, Botswana, Julai 30 na 31, ili kutathimini matokeo ya ripoti mpya kuhusu matatizo yanayowakabili vigori na vijana kuhusiana na afya na elimu ya jinsia.Mkutano huo ambao umeitishwa na shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya ukimwi UNAIDS na lile la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, utafunguliwa na mama Salma Kikwete,mke wa Rais waTanzania.

Ikikadiriwa vijana 52 wanaambukizwa virusi vya HIV kila saa moja, Afrika Mashariki na Kusini inasalia kuwa kitovu cha maambukizi ya HIv duniani.

Elimu na upatikanaji wa huduma za taarifa vinachukuliwakamanyenzo muhimu kwa ajili ya kukabiliana na hali hii. Ripoti hiyo iliyopangwa kutolewa mwezi Oktoba iitwayo “Vijana leo, kuwa tayari kwa ajili ya kesho”inawakilisha takwimu kutoka nchi 21.

Wataalamu watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja na wataalamu na watunga sera kutoka sekta za elimu, afya ya uzazi na haki, ukimwi na maendeleo. Watatathimini matokeo ya ripoti na athari zake.