Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA kuandaa maonyesho juu ya ndoa za utotoni

UNFPA kuandaa maonyesho juu ya ndoa za utotoni

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu linatazamia kuratibu maonyesho ya wazi yatayotanyika Washington kueleza namna vitendo vya kuwaozesha watoto wa kike ambao hawajafikia umri wa kuolewa.UNFPA inasema kuwa kila mwaka zaidi ya wasichana 39,000 wenye umri wa chini ya miaka 18 huolewa jambo ambalo imesema kuwa ni uvunjifu wa haki za binadamu.

Maonyesho hayo yatatawaliwa na picha zilizochukuliwa kutoka sehemu mbalimbali duniani na baadaye kufuatiwa na majadiliano kutoka kwa wawakilish wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na vyama vingine vya kitaaluma.

Kulingana na UNFPA, karibu wasichana milioni 16 wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 15-19 hujifungua kila mwaka na hivyo kuleta kitisho juu ya usalama wa afya zao.