Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wafungua ofisi ya masomo ya utafsiri huko Nairobi

Umoja wa Mataifa wafungua ofisi ya masomo ya utafsiri huko Nairobi

Ufunguzi rasmi wa ofisi inayojulikana kama InZone yenye madhumuni ya kufundisha tafsiri ya lugha mbali mbali barani Afrika umefanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kenya. Mafunzo haya yanalenga wale wanaohudumu katika nchi ambazo zimekumbwa na vita, na athari zinazoletwa na hali hiyo. Kufunguliwa kwa ofisi hiyo kunasisitiza umuhimu unaopewa na Umoja wa Mataifa juu ya lugha na matumizi yake katika kukuza amani , usalama na maendeleo. Ufunguzi huo unafuatia uamuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi (UNON) mwaka jana Bi Sahel-Work Zewde wa kufungua kituo cha Kutafsiri cha nchi za Afrika (PAMCIT) kwenye ofisi hizo. Afisa wa Habari wa Umoja wa Mataifa Nairobi, Irene Mwakesi, amepata fursa ya kumhoji mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo Rajab Luhangela David kutoka DRC .

(MAHOJIANO NA RAJAB LUHANGELA DAVID))