UNRWA yakagua madarasa shuleni eneo la mashariki ya kati

24 Julai 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeendesha utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha York cha Uingereza kuhusu shughuli za darasani katika maneneo matano ambapo Shirika hilo linatoa huduma.Mapema mwezi Julai waakilishi kutoka  maeneo liliko UNRWA walikutana mjiniAmman kujadili matokeo ya utafiti huo na athari zake kwa mifumo ya elimu ya UNRWA na kwa zaidi ya wakimbizi 490,000 wa Kipalestina linaowahudumia.

Kwenye utafiti huu UNRWA ilikagua jumla ya madarasa 230 nchini Lebanon,Syria na Ukanda wa Gaza pamoja na Ukingo wa Magharibi. Katika madarasa haya yote mafunzo yote yalirekodiwa. Utafiti wote kuhusu hali  ndani ya madarasa yanayosimaiwa na Shirika la UNRWA utakamilika ifakapo mwishoni mwa mwezi Agosti. 

Matokeo ya utafiti huo yatatumika katika kushughulikia zaidi sehemu zinazohitaji kuboreshwa  hasa mifumo ya elimu.