Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Duru nyingine ya mabadiliko yahitajika kwa Uchina kuendelea kufanikiwaIMF:

Duru nyingine ya mabadiliko yahitajika kwa Uchina kuendelea kufanikiwaIMF:

Uchumi wa Uchina unatarajiwa kukua kwa asilimia 7 na robo tatu kwa mwaka huu , ikiwa ni sawa na kiwango cha mwaka jana lakini hatari kidogo imejitokeza wamesema wachumi wa shirika la fedha duniani IMF.

Katika ripoti yao kuhusu uchumi wa China wachumi hao wamesisitiza umuhimu wa mabadiliko ili kupata walaji zaidi na ukuaji endelevukatika kusonga mbele.Ripoti inasema ukuaji wa uchumi wa China tangu mdororo wa uchumi wa mwaka 2008 umekaribisha mahitaji makubwa duniani na hatua kubwa kusawazisha akaunti zake za nje . Lakini ripoti imeonya kwamba mfumo wa shughuli za kiuchumi kwa taifa hilo la pili kwa uchumi mkubwa duniani umejikita saana kwenye uwekezaji na madeni na kuiweka sekta ya fedha, serikali za kikanda na mfumo wa biashara nyumbani katika hali ya sintofahamu.

Kwa mujibu wa IMF serikali ya Uchina imetangaza mabadiliko na malengo ya sera kwa mwaka 2013 ambayo yatashughulikia hatari na kuweka sawia hali ya uchumi, lakini ripoti imeshauri kwamba hatua maalumu zichukuliwe na kutekelezwa kwa utaratibu.