Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakutana kuhusu Sudan na Sudan Kusini

Baraza la Usalama lakutana kuhusu Sudan na Sudan Kusini

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo wanafanya mikutano kuhusu nchi za Sudan na Sudan Kusini. Kikao cha Baraza hilo cha asubuhi kwa saa za New York kimefanywa faraghani, lakini baadaye kitafanyika kikao cha wazi, ambako ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu Sudan Kusini itawasilishwa.Kikao cha mchana pia kitaangazia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO. Tutakuletea habari zaidi pindi zinapoibuka.