Kiwango cha uzalisahi nafaka kuongezeka mwaka 2013-FAO

11 Julai 2013

Kiwango cha uzalishaji wa nafaka duniani kinatazamia kuweka historia ya aina yake duniani katika msimu wa mwaka 2013, wakati hali ikiwa hivyo hali ya ukosefu wa chakula inatazamiwa kuwa mbaya zaidi nchini Syria, Afrika ya Kati na Afrika Magharibi.(Taarifa zaidi na George Njogopa)

Uzalishaji wa nafaka unakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 7 katika kipindi cha mwaka 2013, hali ambayo ni ya kutia matumaini ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2012 hatua ambayo wachungizi wa mambo wanaona kuwa itasaidia pakubwa kuimarisha masoko kwenye msimo wa mwaka huu na ule unaokuja.

Makadirio hayo ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la chakula na kilimo FAO, ambalo limechapisha ripiti yake inayoangazia hali ya uzalishaji wa chakula kwa mwaka huu.

Katika ripoti yake hiyo FAO imesema kuwa ongezeko hilo la asilimia 7, kutaifanya dunia kufikisha tani milioni 2,479 za nafaka ikiwa ni rekodi mpya ambayo hajawahi kushuhudiwa.

Pia FAO inasema kuwa, uzalishaji wa ngano unatazamia kufikia tani milioni 704 million ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.8 kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ikilinganishwa na kile kilishohudiwa misumu iliyopita.

Wakati hali ikiwa hivyo, ripoti zinaonyesha kuwa, hali ya uzalishaji wa ngamo umeanguka vibaya nchini Syria kutokana na machafuko yanayoendelea sasa. Maeneo mengine ikiwemo Afrika ya Magharibi nayo yanatazamiwa kuandamwa na mgogoro wa ukosefu wa chakula.