Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na wawakilishi wa Bolivia, Cuba, Ecuador, Nicaragua na Venezuela

Ban akutana na wawakilishi wa Bolivia, Cuba, Ecuador, Nicaragua na Venezuela

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa anaelewa hofu ilotokana na tukio hilo la kusikitisha, na kusema kwamba alifurahia kuwa halikusababisha madhara yoyote kwa usalama wa rais Morales na ujumbe wake. Ameongeza kuwa ni muhimu kuzuia kutokea kwa matukio kama hayo siku zijazo.

Bwana Ban amesema kiongozi wa taifa na ndege yake hawapaswi kuhatarishwa. Ameelezea matumaini yake kuwa serikali zote husika zitajadili hali hii vyema na kwa kuaminiana, pamoja na kuheshimu kikamilifu matakwa yote halali husika na kudumisha uhusiano mwema baina ya mataifa.