Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka vikwazo vya kuwafikia wanaohitaji msaada viondolewe Syria:

WHO yataka vikwazo vya kuwafikia wanaohitaji msaada viondolewe Syria:

Shirika la afya duniani WHO limetoa wito wa kutokuwepo na vikwazo vyovyote vya kuwafikia watu wnaohitaji msaada wa kibinadamu ikiwemo msaada wa madawa nchini Syria.Shirika hilo limesema hatari ya kuzuka magonjwa ya mlipuko yakiwemo yanayosababishwa na maji kama kuhara, homa ya matumbo au Typhoid, kipindupindu na hepatitis ni kubwa.

Watu wanaokimbia huku na huko wanakabiliwa na mazingira mabaya ya kiafa na kuwa katika hatari ya mlupuko wa magonjwa hayo hasa wakati huu wa majira ya joto. Ongezeko la maradhi ya surua na magonjwa mengine ya kuambukiza limebainika miongoni mwa wakimbizi wa ndani.

WHO inasema pia kumearifiwa ongezeko la kmagonjwa ya kuhara, hususani katika maeneo ya vijijini nje ya Damascus ya

Idlib, Homs, Aleppo na Deir Ez-Zor.Wakati huohuo chanjo ya kitaifa imeshuka kutoka asilimia 95 mwaka 2011 hadi asilimia 45 mwaka huu.

WHO imeandaa vifaa vya msaada ikiwemo madawa ili kushughulikia maradhi hayo. Pia imeandaa mpango wa dharura ili kuhakikisha inakabiliana na mlipuko wowote utakaotokea. Mpango huo wa dharura unaratibiwa kwa ushirikiano na washirika wa WHO katika kitengo cha WASH.