Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM: Ongezeko la kasi la watu mijini ni tishio kwa maendeleo endelevu

UM: Ongezeko la kasi la watu mijini ni tishio kwa maendeleo endelevu

Utafiti mmoja  ulioendeshwa na Umoja wa Mataifa kupitia kitendo chake cha Uchumi na Jamii umeonyesha  kuwepo haja ya kuanzisha mikakati mipya ili kukabiliana na changamoto la watu wengi kuhamia mijini kunakochangia na mambo mbalimbali ikiwemo mahitaji ya nishati ya umeme, maji, huduma za umma na elimu.George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kwa mujibu wa utafiti huo, kiasi cha watu bilioni 6.25 watakuwa wanaishi katika maeneo ya mijini hadi kufikia mwaka 2050 na nusuyaowanaelezwa kuwa watakuwa wakiishi  kwenye maeneo ya ovyo ovyo wakikosa huduma muhimu ukiwemo majisafina salama, miundombinu bora, umeme na kukosa huduma za afya na elimu.Kama hiyo haitoshi utafiti huo unatoa zingatio kwenye eneo la chakula ukitaka kuwepo mabadiliko makubwa kwenye ulaji wa chakula ili kukaribisha umlingano wa ulaji chakula hatua ambayo itasaidia kuepuka kile kinachoelezwa kundi kubwa la chakula kutupwa majalalani.

Shamshad Akhtar  ni msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusiana na maendeleo ya Uchumi.

 (SAUTI YA SHAMSHAD AKHTAR)

“ Shaka yetu kubwa ni kwamba mtu mmoja kati ya watu nane duniani kote bado wanaandamwa na tatizo hili ukosefu wa chakula. Katika hali ya sasa agenda ya kubadilisha mwelekeo ili kuwaokoa watu maskini wanaokabiliwa na tatizo la njaa ifikapo mwaka 2015  inaweza isitimie katika eneo la Kusin mwa Jangwa la Sahara.

Na kwa ongezeko la watu bilioni 2.4 ifikapo mwaka 2050, hali ya upatikanaji wa chakula italazimika kuongezeka kwa asilimia 70 duniani kote.Kutokuwepo kwa uhakika na kiwango duni cha upatikanaji wa nishati kunaendelea kutia shaka hasa katika maeneo ambayo ni ya watu maskini ambao kiasi kikubwa wamejiari wao wenyewe ama wanaendesha ujasiliamali mdogo mdogo.

Hali jumla iliyowasilishwa kwenye ripoti hii inaonyesha kuwepo ukosefu mkubwa wa mipango ya sera ya endelezajiwa nishati ya umeme, jambo ambalo litafanya kiasi cha watu bilioni 2.4 wataendelea kutegemea vyanzo vya kale kama chanjo mbadala cha kupikia."