Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano kati ya Serikali na waasi ndio suluhu kwa mzozo Darfur:UNAMID

Ushirikiano kati ya Serikali na waasi ndio suluhu kwa mzozo Darfur:UNAMID

Hali ya Usalama Darfur bado ni tete kwa sababu ya mzozo kati ya serikali na waasi, mizozo baina ya makabila nayo ni changamoto lakini mazungumzo yatakayojumuisha pande zote ndio njia pekee ambayo itaweza kuleta suluhu ya kudumu katika kutokomeza mzozo ambao umeshuhudiwa Darfur nchini Sudan kwa karibu miaka kumi .Grece Kaneiya na taarifa zaidi(RIPOTI YA GRECE KANEIYA)

Kauli hiyo imetolewa na Meja Jenerali Wynjones Mathew Kisamba kaimu Kamanda wa kikosi cha UNAMID alipofanya mahojiano rasmi na Radio ya Umoja wa Mataifa

(Sauti ya Meja Jenerali Kisamba)

Ameongeza kuwa licha ya kwamba hadi sasa kundi la waasi halijaweza kung'atua serikali kutoka madarakani, kwa upande mwingine serikali imeshindwa kumaliza shughuli za kundi hilo na cha msingi ni kwamba UNAMID na Jumuiya ya Kimataifa wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta suluhu ya kudumu Darfur kwani wanaoumia zaidi ni Watoto na akina mama.

(Sauti ya Meja Jenerali Kisamba)