Nchi wanachama zatakiwa kutekeleza mkataba wa kupinga utesaji:Ban

26 Juni 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongeza juhudi za kuwasaidia waathirika wa utesaji na unyama wa aina nyingine, vitendo visivyo vya kiutu na adhabu za kudhalilisha.

Amesema wakati dunia ikiadhimisha siku ya kuunga mkono waathirika wa utesaji ni muhimu kuimarisha mtazamo unaowagusa waathirika na unaojumuisha masuala ya jinsia.

Amesema hayo yote ynatiwa nguvu na kupitishwa kwa azimio mwaka huu na baraza la haki za binadamu linalojikita katika msaada kwa waathirika wa utesaji.

Ban amezitaka nchi zote wanachama kutekeleza kikamilifu mkataba wa kupinga utesaji na kuunga mkono mfuko wa hiyari wa Umohja wa mataifa wa kuwasaidia wahanga wa utesaji.

Ameongeza kuwa ni muhimu kushirikiana kutokomeza tatizo hilo kote duniani na kuhakikisha kwamba nchi zinatoa msaada kwa waathirika.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud