Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto walio ukimbizini wakabiliwa na ndoa za mapema: UNHCR-Tanzania

Watoto walio ukimbizini wakabiliwa na ndoa za mapema: UNHCR-Tanzania

Ripoti ya mwelekeo wa wakimbizi duniani kwa mwaka 2012 imetaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Tanzania linasema kuwa kwa sasa wakimbizi wako katika kambi ya Nyarugusu ikiwa idadi yao ni Elfu sitini na Wanane.

Bi. Joyce Mends-Cole Mkuu wa UNHCR nchini humo anasema kuwa miongoni mwa wakimbizi hao ni watoto ambao hail yao ya maisha inatia wasiawsi ofisi yake kwa kuwa wanashindwa kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu na badala yake watoto wa kike wanajikuta katika mtego.

(SAUTI YA Bi. Mends-Cole)