Mpiga mbizi mashuhuri Lewis Pugh ateuliwa kuwa mlezi wa UNEP wa masuala ya bahari:

19 Juni 2013

Bwana Pugh wakili wa masuala ya bahari kutoka Uingereza ni mtu wa kipekee kuwai kumaliza mbizi ndefu zaidi kwenye kila bahari ya dunia, Mwaka 2007 alipiga mbizi  baharini kaskazini mwa dunia kama hamasisho kuhusu kuyeyuka kwa barafu kwenye bahari ya Arctic na mwaka 2010 akapiga mbizi kwenye ziwa mpya katika mlima Everest kutoa hamasiho kuhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye milima ya Himalaya.

Mwaka ujao bwaa Pugh ataanza safari ya miaka mitatu  ambapo atavuka bahari   18. Akiwa kwenye safari hiyo atakuwa akitangaza  wajibu wa Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa kwenye kampeni ya kutaka kulindwa kwa sehemu za maji.

Mpiga mbizi huyo amesema kuwaa kwa kipindi cha miaka 27 ameshuhudia bahari zikibadilika. Anasema ameona theluji ikiyeyuka akisema kuwa mabadiliko hayo yote yamesababishwa na mwanadamu.