Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hungary inataka kubinya uhuru wa vyombo vya maamuzi: Pillay

Hungary inataka kubinya uhuru wa vyombo vya maamuzi: Pillay

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay leo ameitolea mwito serikali ya Hungary kusitisha mara moja mfululizo wa matukio ya urekebishwaji wa katiba, matukio ambayo yanashutumiwa vikali na jumuiya za kimataifa kwa maelezo kuwa yanabinya uhuru wa kikatiba. Wito huo umekuja katika wakati ambapo baraza la ushauri barani Ulaya likiwa limetoa ripoti kali kuhusiana marekebisho ya katiba nchini humo, marekebisho ambayo yanatajwa kubana baadhi ya taasisi za maamuzi ikiwemo mahakama. Pillay ametaka kuheshimiwa kwa mkataba waVeniceambao pamoja na mambo mengine unataka uhuru wa mahakama kutoingiliwa na mamlaka nyingine yoyote. Amesema jaribio lolote la kuzibana mhimili mwingine wa dola halikubaliwa na kuitakaHungarykuanchana mara moja za zoezi lake la marekebisho ya katiba