Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Koenders akaribisha utiwaji saini makubaliano nchini Mali.

Koenders akaribisha utiwaji saini makubaliano nchini Mali.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Mali aliye pia Mkuu wa Ujumbe wa kuimarisha amani nchini humo MINUSMA Albert  Koenders amekaribisha utiwaji saini wa makubaliano ya awali ya uchaguzi wa rais na mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Mali,  chama cha National Movement for the Liberation of Azawad (MNLA) na baraza kuu la Umoja wa Azawad yaliyofanyika leo Juni 18 Ouagadougou, Burkina Faso. Bwana Koenders amesema makubaliano hayo yanaonyesha hatua muhimu katika mchakato wa kuimarisha amani nchiniMalina kupongeza vyama ambavyo vimeweka tofauti zao pembeni na kufanya kazi kwa manufaa ya nchi na watu.

Amesema hii ni hatua ya kwanza na muhimu kwa kuwa wahusika wametazama mbele na kuendeleza juhudi zao kwa kushikamana katika kutekeleza kwa vitendo makubaliano hayo yanayotarajiwa kuanza hima kwa namna yalivyoratibiwa na kwa amani. Hata hivyo kinadharia pande hizo bado hazijajadili maswala ya kiufundi kuhusu usalama, kurejea kwa utawala, huduma muhimu kwa watu wa ukanda wa Kidal na maandalizi kwa ajili ya uchaguzi ujao wa  nne wa rais.