UNHCR yachapisha utafiti wake kuhusu ukosefu wa makazi kwa wakimbizi walioko Poland, Bulgaria na Slovakia

7 Juni 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UHNCR leo limechapisha tafiti tatu ambazo zimeangazia madhira wanayokumbana nayo jamii za wakimbizi waliko katika nchi za Poland, Bulgaria na Slovakia.Tafiti hizo zenye kichwa cha habari kisemacho nyumbani kwangu ni wapi? zimemulika suala la ukosefu wa makazi katika nchi hizo tatu suala ambalo limebainika kuwa ni moja ya tatizo kubwa linalowakabili wakimbizi na wale wanaoomba hifadhi.

Kwa mfano nchini Poland utafiti huo umebaini kuwa kiasi cha asilimia 10 ya wale wanaopata hifadhi nchini humo wanaishi maisha ya kubangaiza kwa kukosa makazi ya kudmu wakati huko Bulgaria suala la kupata makazi ni tatizo sugu kwa raia wengi wanaoomba hifadhi.

Kuhusu Slovakia utafiti huo unasema kuwa maeneo mengi ambayo yalikuwa yameaandaliwa kwa ajili ya waomba hifadhi yalikuwa hayana watu lakini utafiti huo haukuweza kueleza sababu ya hali hiyo.