Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa mpangilio wa kukabiliana na uzito wa juu wa mwili miongoni mwa watoto

WHO yatoa mpangilio wa kukabiliana na uzito wa juu wa mwili miongoni mwa watoto

Nchi nyingi zenye kipato cha chini na cha wastani zimetupilia mbali masuala ya uzito wa mwili kupita kiasi na athari zake kwa afya wakati kukiwa na sera za kukabiliana na ukosefu wa lishe wakati pia ambapo kuna ukosefu wa sera za kuzuia magonjwa yanayosababishwa na uzito wa juu wa mwili kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka kwa Shirika la afya duniani WHO. Zaidi ya asilimia 75 ya watoto wenye uzito wa juu wanaishi kwenye nchi zinazoendelea hasa za bara la afrika huku idadi hiyo ikiongezeka maradufu kwa muda wa miaka 20 iliyopita. Watoto kama hao wanaweza kukua wakiwa na uzito wa juu wakiandamwa na hatari ya kukumbwa na maradhi kama vile kisukari. Ili kukabilina na hali hii WHO imetoa mpangilio wa hatua 24 za lishe kuhusu njia amabzo nchi zinaweza kutumia ili kuboresha viwango vya lishe ya watu kwa kuzuia ukosefu wa lishe na uzito wa juu wa mwili ikiwemo kwa kuboresha lishe ya akina mama wajawazito na wanaonyonyesha, kushauri akina mama kunyonyesha watoto wa kipindi cha miezi sita ya kwanza na hadi miaka miwili na kuwapa vyakula vigumu wawatoto wachanga.